Kiongozi wa upinzani Somaliland ashinda uchaguzi wa rais
19 Novemba 2024Matokeo hayo ni kwa mujibu wa kituo cha habari cha mtandaoni cha Garowe ambacho, kimeinukuu tume ya uchaguzi ya Somaliland. Kiongozi wa upinzani katika jimbo la Somaliland,Abdirahman Cirroameshinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika wiki iliyopita. Matokeo hayo ni kwa mujibu wa kituo cha habari cha mtandaoni cha Garowe ambacho, kimeinukuu tume ya uchaguzi ya Somaliland. Kwa mujibu wa matokeo hayo kimesema kwamba kiongozi huyo wa upinzani wa chama cha Waddani amepata asilimia 64 ya kura dhidi ya rais aliyoko madarakani Muse Bihi Abdi aliyepata asilimia 35. Somaliland ni jimbo lenye utawala wake wa ndani baada ya kujitenga na Somalia tangu mwaka 1991,japo haijatambuliwa na nchi yoyote, hatua inayolifanya jimbo hilo kushindwa kupata ufadhili wa taasisi za kifedha za kimataifa na raia wake milioni 6 kushindwa kusafiri.