MichezoZambia
Kombe la Dunia: Zambia itamkosa Chanda dimbani
21 Julai 2023Matangazo
Hii ni baada ya mshambuliaji wake muhimu Grace Chanda kuondolewa kwenye kikosi kinachoshiriki michuano hiyo.
Hili ni pigo la pili kwa kikosi cha kocha Bruce Mwape baada ya mlinda lango nambari moja Hazel Nali kuumia goti na nafasi yake kuchukuliwa na chipukizi Leticia Lungu.
Soma pia: Michuano ya Kombe la Dunia la wanawake yaanza rasmi
Daktari wa timu hiyo Faith Chibeza hakueleza zaidi sababu ya kutokuwepo kwa mshambuliaji huyo, lakini duru zimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba amelazwa akipata matibabu.
Chanda ni nahodha wa zamani wa kikosi hicho na mchezaji muhimu aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuliinua kwa haraka soka la kimataifa nchini humo katika miaka ya karibuni.