Kura ya maoni yaonesha Putin anaweza kushinda asilimia 82
12 Machi 2024Matangazo
Matokeo hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa wapiga kura wanaostahiki uliofanywa na taasisi ya utafiti wa maoni ya VCIOM yenye kuegemea upande wa mamlaka.
Wagombea watatu wa upinzani, ambao wanamuunga mkono waziwazi Putin au wanaofuata mwelekeo wa serikali ya Kremlin, wanaonekana kuwa na uwezo wa kupata asilimia 5 na hadi 6 kila mmoja.
Kura za maoni za Urusi zinatazamwa kama mbinu muhimu ya serikali kufanya tathmini ya ufanisi wa propaganda za Kremlin, kwa zingatio la vyombo vya habari vya umma. Televisheni ya serikali inayodhibitiwa na Kremlin, inatazamwa zaidi na wazee wa Kirusi katika maeneo ya vijijini, wanamwonyesha Putin kama mtu asiyekuwa na mbadala.