Lewandowski ashinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora
18 Desemba 2020Nahodha huyo wa Poland ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA Mwanaume katika mwaka wa 2020 baada ya mabao yake 55 ya msimu kuisaidia Bayern Munich kunyakua mataji ya kimataifa na ya nyumbani.
Lewandowski alipata kura 52 dhidi ya 38 alizopata Lionel Messi wakati Cristiano Ronaldo akipata 35. Hafla ya tuzo hiyo ilifanyika Zurich kwa njia ya video lakini Rais wa FIFA Gianni Infantino alikwenda hadi Munich kumkabidhi binafsi Lewandowski tuzo yake. Lucy Bronze wa Uingereza alishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.
Alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Olympique Lyonnais kabla ya kuhamia Manchester City. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alimpiku Mjerumani mwenzake Hansi Flick wa Bayern Munich na Marcelo Bielsa wa Leeds katika tuzo ya kocha bora. Manuel Neuer alishinda tuzo ya kipa bora.
afp, dpa,reuters, dpa