Mabomu yaua zaidi ya 50 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 40 Algeria
11 Desemba 2007Watu zaidi ya 50 wameuawa na wengine wasiopungua 40 kujeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu ya mabomu yaliyotokea katika leo katika mji mkuu wa Algeria.
Milipuko miwili ya mabomu imetokea mjini Algiers ambapo duru za usalama za Algeria zimesema watu zaidi ya 50 wameuawa.Wengine 43 wamejeruhiwa.Mlipuko wa pili umetokea dakika 10 baada ya ule wa kwanza kwa mujibu wa habari kutoka huko.
Bomu la kwanza limeripotiwa kutokea nje ya jengo la mahama kuu ya Algeria.Haikufahamika haraka ikiwa bomu ambalo limeilipua basi ya wanafunzi lilikuwa ndani ya basi hilo au nje yake. Bomu lingine linasemekana kutokea karibu na makao makuu ya ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohisika na wakimbizi ya UNHCR.
Jengo la umoja wa mataifa liliharibiwa na mlipuko huo.Msemaji wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNDP,amenukuliwa kusema kuwa alikuwa anapata shida kuwasiliana na wafanyakazi wengine katika jengo hilo baada ya saa tatu unusu za asubuhi saa za Algeria wakati wa mlipuko.
Duru za serikali ya Algeria zinasema kuwa mabomu yote yalikuwa ndani ya magari, mojawapo ikiwa na dereva ndani yake. Hata hivyo walioshudia wamekiambia kituo kimoja cha televisheni cha BFM kuwa, basi laonekana kama limelipuliwa na bomu iliokuwa ndani ya basi hilo.Mlipuko wa basi umesababisha wahanga wengi.Hakuna kundi ambalo limejitokeza kuhusika na tukio hilo, hata hivyo kundi la Al Qaeda,tawi la kaskazini magharibi mwa afrika limehusika na mashambulizi kadhaa ya mabomu nchini humo tangu mwanzo wa mwaka huu.Zamani lilikuwa likijulikana kama kundi la kisalafi la Salafist Group for Preaching and Combat-GSPC- na liliunganishwa katika mtandao wa Al-Qaida mwezi januari.
Tume ya Ulaya imeliláani shambulio hilo na kuliita kama tendo la kinyama na kutoa mkono wa pole kwa wahanga.Katika taarifa iliotolewa na kamishna wa mashauri ya kigeni ya Umoja wa Ulaya-Benita Ferrero-Walder, imesema kuwa inatumai waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria. Shambulio la leo ndilo la sita mwaka huu kutokea nchini Algeria, lakini ndilo baya zaidi kwa kuwauwa watu wengi.Shambulio la Septemba 6 liliwauwa watu 32 na kuwajeruhi 45 katika kambi ya walinzi ya Delly katika mji wa bandari wa Kabylie,ulioko umbali wa kilomita 70 mashariki mwa mji wa Algiers.
Watu wasiopungua 50 wameripitiwa kuuawa na 43 kujeruhiwa shambulio la jumanne . Miongoni mwa majeruhi ni raia wa kigeni bila kufafanua ni wa kutoka wapi. Yeye waziri mkuu wa Uhispania- Jose Luis Rodriguez ,wakati akilaumu shambulio hilo, serikali yake imesema haina habari za ikiwa miongoni mwa wahanga wa mabomu hayo kuna raia wake.Nae rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amelaani shambulio hilo.