JamiiIsrael
Maelfu waandamana Israel dhidi ya mageuzi ya Mahakama
13 Februari 2023Matangazo
Mageuzi hayo yaliyokaribia kuidhinishwa kupitia mfululizo wa kura bungeni, yamechochea ukosoaji mkubwa kwamba yatalipa bunge mamlaka yasiyoweza kudhibitiwa.
Wakiwa wamebeba vijibendera vya Israel, maelfu ya waandamanaji hao walibeba mabango yenye ujumbe usema, iokoe demokrasia ya Israel na kwamba ulimwengu mzima unatizama.
Katika hotuba ya nadra kwa taifa usiku wa kuamkia leo, rais wa Israel Isaac Herzog aliangazia mpango wa mageuzi huku akitahadharisha kuwa Israel iko katika hatari ya kuporomoka kisheria na kijamii.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu na washirika wake wanasema mageuzi ni muhimu kurekebisha ukosefu wa usawa wa mamlaka kati ya wawakilishi waliochaguliwa na mahakama ya juu zaidi nchini humo.