Maelfu waandamana kushinikiza mabadiliko ya uongozi Valencia
10 Novemba 2024Waandamanaji hao walioingia barabarani Jumamosi wanapinga namna serikali ilivyoshughulikia maafa hayo, siku kumi na moja baada ya uharibifu mkubwa katika eneo hilo. Maandamano hayo yaliitishwa na mashirika 65 zikiwemo taasisi za kiraia na vyama vya wafanyakazi.
Soma zaidi: Uhispania yatenga zaidi ya $ bil 10 kusaidia waathiriwa mafuriko
Baadhi ya waandamanaji walisikika wakisema "wauwaji wajiuzulu" huku wengine wakiwa na mabango yaliyomtaka kiongozi wa serikali ya eneo hilo, Carlos Mazon ajiuzulu.
Mamlaka zinakadiria kuwa waandamanaji 130,000 walishiriki katika maandamano hayo ya Valencia. Mapema Jumamosi ofisi ya utawala wa Kifalme ya Uhispania ilitangaza kuwa Mfalme Felipe wa sita atatembelea Valencia ili kufuatilia operesheni za uokoaji na kusafisha maeneo